Monday, January 7, 2013

WAZEE IFINGA SONGEA WATOZWA PESA ZA MATIBABU HOSPITALI

Baadhi ya Wazee niliokutana nao katika Kijiji cha Ifinga Kata ya Matumbi Wilaya ya Songea katika Mkoa wa Ruvuma, wakilalamika kuendelea kutozwa pesa za matibabu wakienda katika zahanati, kituo cha afya na hospitali mbalimbali Songea, japo kuwa wana daftari ambalo limegongwa muhuri wa kutibiwa bure lakini mzee akifika hospitali kupata matibabu akionesha daftari hilo anaambiwa ni lazima kulipia huduma ya afya.
"Tunashindwa kuelewa hii huduma ya bure kwa wazee bado ipo au imefutwa? maana kila ukifika hospitali unaambiwa ulipe pesa ya matibabu, nimefanyiwa upasuaji wa henia nimelipia Tsh. 100,000 sijapewa dawa kwa sababu pesa imekwisha nimeamua kurudi nyumbani nasikia maumivu kweli kwenye mshono," alisema Mzee Rwanda.

0 comments:

Post a Comment