Friday, January 18, 2013

MAJI YAWA DHAHABU RUFIJI

Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Mlanzi katika Wilaya ya Rufiji Mkoa wa Pwani, wakichota maji ya matuzi ya kila siku ya nyumbani kwa shida sana katika kisima kiferu, kwa muda mrefu upatikaji wa maji salama katika kijiji hicho umekuwa wa shida sana, mpaka inawalizimu akinamama na watoto kushinda na kukesha usiku kisimani hapo kusubiri maji.

"Maji ni dhahabu hapa kijijini kwetu nimefika toka saa 5 hasubuhi mpaka sasa saa 10 bado sijapata maji hata ndoo moja na nyumbani nimecha pakavu hakuna maji hata tone, kama kunatokea mtoto anaharisha au mimi mwenyewe sina maji ya kumpa kijisafisha au kumeza dawa, ukifika hapa kisimani unatakiwa kuacha kazi zingine zote usubiri mpaka utakapo pata maji, unasubiri kwa saa tatu unachota ndoo mbili yamekuwa yameisha kisimani unasubiri tena baada ya saa tatu unachota ndoo mbili, tunatumia muda mwingi sana kusubiri maji badala ya kufanyashughuli zingine za kimaendeleo kama kulima na kipindi hiki ndio cha kilimo lakini mashamba yamejaa majani akinamama tuko busy kusubiri maji kisimani," alisema Maimuna Mkima.

Wakazi wa Kijiji hicho wanaiomba Wizara ya Maji na Umwagiliaji kuwachimbia kisima kirefu cha kisasa ili wapate maji kiurahisi na kuondokana na adha ya kushinda na kukesha kisimani kila siku, badala ya kuangalia maendeleo ya kilimo katika mashamba yao.

0 comments:

Post a Comment