Tuesday, January 15, 2013

HII NI HATARI KWA WALAJI WA SAMAKI

Msaidizi wa Mvuvi akiburuza samaki aina ya kitaa katika Soko la Feri Jijini Dar es salaam, uburuzaji wa samaki kwa aina hii ni hatari sana kwa afya za binadamu. Afisa Afya wa Sokoni Feri Kesia Bernard alisema kuwa uchuuzi wa samaki kwa kuburuza sehemu ambayo sio safi na salama ni kinyume cha sheria na utaratibu wa kubeba samaki hapa sokoni, mvuvi akikamatwa anafanya kitendo hicho anatozwa faini ya Tshs. 10,000 hadi 50,000.Kwa siku tunawakamata wavuvi kuanzi watano hadi saba wanaofanya uchuuzi wa samaki kwa kuwaburuza chini.
Meneja wa Soko hilo la Feri Charles Kapongo alisema kuwa tatizo la ubebaji wa samaki bila ya kufuata taratibu na sheria za soko la samaki zimekithiri hapa sokoni, hii inatokana na wadau wa samaki kukaidi kubeba samaki hao katika vikapu lakini pia ukosefu wa matoroli maalumu ya kubebea samaki kwa muda wa miaka 9 sasa ndio sababu kubwa ya kukithiri kwa uburuzaji wa samaki.
"Tunaiomba Halmashauri ya Wilaya ya Ilala kutununulia matoroli maalumu ya kubebea samaki ili samaki achukuliwe katika mazingira safi na salama,".
Mahitaji ya toroli kwa sasa ni 20 hadi 25, apo awali toroli hizo zilikuwa zinakodishwa kwa siku ni Tshs. 300.

0 comments:

Post a Comment