Hii
ndio hali halisi utakayo kutana nayo kilometa 660 kutoka Dar es Salaam na
kilimeta 122 kutoka Nachingwea. Katika kijiji cha Kiegei kila tarehe 25 ya
mwisho wa mwezi, baada ya mnada wa bidhaa mbalimbali za kilimo kama chakula na
vifaa vya nyumbani kama vyombo.
Watu
wengine, wekiwemo watoto wa shule za msingi huuziana mabusu na wafanyabiashara
wa mnada huo, kusababisha kukatisha masomo kwa baadhi ya wanafunzi kwa kushika
ujauzito na wengine kupata magonjwa ya
kuambukiza kama gono, kaswende na Ukimwi.
Baada
ya kuuza bishaa zao mbalimbali katika mnada
huo, unaohusisha wafanyabiashara kutoka katika wilaya za jirani kama
Liwale, Tunduru na Masasi, wafanyabiasha wa Kiegei huingia katika vibanda vya
sinema, mathalani kuangalia filamu mbalimbali, lakini humo ndani ya vibanda
filamu hutumia pesa zao kununua ngono kutoka kwa watoto.
Sera
ya Maendeleo ya Mtoto ya mwaka 2008 inalenga kuhakikisha kwamba watoto wote
wanastawi na kuwa na maisha bora, kutokana na kupatikana kwa haki zao za msingi
ambazo ni kuishi, kuendelezwa, kulindwa na kushirikishwa katika mambo
yanayowahusu bila ua ubaguzi wa hali yoyote.
Kwa
mujibu wa sera hiyo, mtoto ni yule mwenye umri wa chini ya miaka 18. Mtu yeyote
mwenye umri wa chini ya miaka 18 anastahili kulindwa na familia yake pamoja na
wanajamii wanaomzunguka ili kumuangalia ukuaji wake uwe wenye usalama zaidi.
Madhara
ambayo anaweza kuyapata mtoto kama hajapata uwangalizi kutoka katika familia
yake na jamii inayomzunguka ni, kuathirika kiafya, kiakili, kimwili, kihisia na
kijinsia.
Pia
pale ambapo maendeleo ya mtoto yanavurungwa, ni pale uhai wa mtoto uko
hatarini pamoja na utu wa mtoto unapokosekana.
Sheria
ya kimataifa ya mwaka 2009 ya kutetea watoto kutoka umoja wa mataifa inaeleza
kuwa, mtoto wa chini umri wa miaka 18 anatambulika kama mtoto kidunia na
anastahili kulindwa na familia yake na kupewa mahitaji muhimu kama chakula
bora, maradhi, nguo na elimu bora, mtoto huyu atakiwa kuanza kujitegemea yeye
mwenyewe au kuachiwa huru kufanya ngono zembe na ajira majumbani na mashambani
ili alishe familia hairuhusiwi kimataifa.
Lakini,
ukitembelea vibanda vya sinema vya kijiji cha Kiegei kuanzia saa 12.00 jioni,
utawakuta watoto wa kike, wenye umri kuanzia 10 hadi 14, katika shuguli mbali
mbali za kutafuta hela kwa kuuza ngono.
Siku
ya tarehe 25 Januari, 2013, ambayo ilikuwa ni siku ya ijumaa, zikioneshwa
sinema za kivita mbili, wasichana wapatao 10 walionekana ndani ya kibanda cha
sinema kilichopo katika kijiji cha Kiegei, wakipakwatwa na kushikwa-shikwa na
wanaume wenye umri mkubwa.
Saa
6:00 usiku, kila mtoto alitoka na mwanaume na kuelekea sehemu mbalimbali kama
vyoo vya shule ya msingi Kiegei, uwanja wa mpira na wengine kwenye meza za
mchezo wa pool, iliyopo katika Soko dogo la kijiji cha Kiegei na wengine
pembezoni mwa jengo la Kanisa.
Mtoto
huyo na mwanaume mtu mzima wakiwa katika meza ya mchezo wa pool, wakaanza
kufanya ngono mbele ya macho yangu, bila hata ya kuona aibu yoyote, tena bila
hata huruma kama anayefanya naye ngono ni mtoto wa shule ya msingi.
“Kama unaona mwenzio anafaidi na tendo hili la
ngono basi njoo weye mtu mzima ufanye; naona umeshangaa kwa kutoa macho
utazani hujui nini kinachofanyika hapa,” alisema jibaba hilo huku akiendelea
kufanya ngono na kitoto hicho.
Saa
12:00 asubuhi kesho yake, hakukukuwa na mabaki ya kondom katika maeneo haya
yote.
Kwa
mujibu wa wanafunzi wa shule ya msingi Kiegei, wanalipwa kiasi cha sh.500 hadi
sh.2000 kufanya ngono na watu wazima.
“Nimeanza
ngono nikiwa na umri wa miaka 12, kabla hata sijabalehe nafanya ngono na
wanaume wakubwa ambao ni wachimbaji wa madini Mbwemkuru na wafanyabiasha ya
mnada wanaofika kila tarehe 25 ya mwisho wa mwezi, kwa ujila wa Tshs. 500 hadi
Tshs. 2000 kwa siku,” alisema Anna Peter (13) sio jina lake
Wakati
huo huo, mwalimu mkuu wa shule ya Kiegei, Fred Mchekenje, alisema kuwa
wanafunzi wa shule yake bado hawajaanza kufanya ngono kwani bado wadogo sana na
kudai kwamba mambo hayo wanafanya watoto wa mitaani.
“Bado
wadogo sana; hawajaanza kufanya mambo hayo ya kiutu uzima. Wanapenda kusoma na
muda mwingi wako nyumbani wanajisomea wakitoka shuleni,” alisema
Mchekenje.
Mchekenje
alisema kuwa, mwaka 2012 wanafunzi wapatao 29, walifanya mtihani wa kumaliza darasa
la saba, kati ya hao wanafunzi 29 walifaulu kujiunga na kidato cha kwanza
katika shule ya sekondari Kiegei, kati ya hao wasichana 11 na wavulana 18.
Mwaka
2011 wanafunzi walifaulu walikuwa asilimia 70 na wakapata fulsa ya
kujiunga na masoma ya sekondari na vyuo vya ufundi stadi veta.
Asilimia
30 ndio waliobaki mtaani ambao hawakufaulu na kupata nafasi ya kuendelea na
masomo ya sekondari katika shule mbalimbali za sekondari Nachingwea.
Aidha
alisema kuwa matokeo ya darasa la nne yalikuwa mabaya sana kwa mwaka 2012;
waliofanya mtihani walikuwa 95 na waliofaulu ni watoto nane tu. Kati ya hao,
wavulana walikuwa sita na wasicha ni wawili. Kwa mujibu wake, sababu kubwa ya
kufeli ni kutokuwepo kwa vitabu, chaki na upungufu wa walimu; badala ya 15, kwa
sasa wapo watatu.
Mchekenje
alisema kuwa mahudhurio ya watoto wa kike shuleni ni mazuri na hakuna mimba
iliyopatikana kwa miaka saba sasa; mara ya mwisho kumpata mtoto mwenye ujauzito
ni mwaka 2006. Anadhani sababu kubwa ya kupungua kwa mimba shuleni ni kuwepo
kwa somo la elimu lika lililoanza kufundishwa mwaka 2007.
Kwa
mujibu wa Juma Ramadhani, ambaye ni mkazi wa kijiji hicho na mzazi wa watoto
watatu wanasoma katika shule ya msingi Kiegei, mwaka 2012, wanafunzi wawili
walipata mimba wakiwa darasa la sita na kukatisha masomo yao.
Kama
Anna, Salima Musa (sio jina lake) ni mwanafunzi wa shule ya msingi. Mtoto huyu,
amabye ana miaka 11 na yuko darasa la tano katika shule ya msingi Ukombozi
anasema, “Nimezoeya kufanya ngono na watu wazima. Sitaki watoto wa shule
wenzangu kwa sababu wananuka mkojo; nataka wanaume wenye misuri iliyokomaa
kwani ndio nasikia raha zaidi.”
Aziza
Ally (siyo jina lake) aliacha shule mwaka huu, akiwa darasa la sita. Hana ndoto
tena za kwenda shule maana ngono anayofanya ndio inampa uwezo wakuilisha
familia yake kwa sasa.
“Sijawahi
kutumia kondom toka nimeanza kufanya ngono nikiwa darasa la nne. Kwa sasa
nimeamua kuacha shule kwa sababu walimu wameniamba nirudie darasa la tano
badala ya kuwa darasa la sita.
Nimeona bora nifanye ngono ili nijikimu kimaisha
kwa kujinunulia nguo, viatu na mafuta mazuri pamona na kutoa nyumbani pesa ya
chakula. Hapa unaponiona nimetoka kumaliza dozi ya ugonjwa wa gono wiki
moja iliyoisha na sasa niko mawindoni natafuta pesa.”
Baba
yake Aziza aliki kufahamu kwamba mtoto wake anajihusisha na ngono zembe.
“Nimemkanya
asifanye ngono lakini hasikii. Nimeamua kumuacha tuu ila kwa sasa sina huduma
yoyote ninayopa mtoto huyo; anajinunulia mwenyewe nguo za kuvaa, mafuta ya
kupaka na chakula,”alisema Baba yake Aziza.
Kwa
mujibu wa Dk. Kahabi Isangura, mtaalamu wa magonjwa ya kijamii, kuna madhara
makubwa sana kwa mtoto kuanza kufanya ngono katika umri mdogo. Anaweza kupata
mimba na kukatisha ndoto zake za kusoma, anaonekana muhuni pamoja na kukabiliwa
na majukumu makubwa akiwa na umri mdogo.
Dk.
Isangura alisema kuwa madhala ya kiafya ni kama kupata magonjwa ya kuambukiza
yakiwemo ukimwi, gono, kaswende na kisonono. Pia, anaweza kupata kansa ya
kizazi kwa kuanza ngono mapema kwa sababu seli za kingo za uke zinakuwa
hazijakomaa vema, hivyo nirahisi kupata majereha na kuweka ufa ambao
unasababisha kupata kansa ya kizazi akiwa mtu mzima.
Ngono
ya utotoni husababisha vifo vya wajawazito wakati wa kujifungua kwa sababu
mtoto mwenye umri wa chini ya miaka 14 nyonga yake ya uzazi inakuwa bado
haijakomaa kusukuma mtoto wakati wa kujifungua, hivyo basi kunauwezekano mkubwa
wa mtoto huyu kupoteza maisha wakati wa kujifungua.
Kwa
mujibu wa takwimu zilizotolewa na Mganga wa Zahanati ya Kiegei Olafu Chinguile,
mwaka 2011 wagonjwa 48 walifika wakiwa wanaumwa magonjwa ya Kaswende na Gono;
kati ya hao watoto walikuwa 5.
Mwaka
2012 wagonjwa waliofika katika zahanati yake wakiwa wanaumwa magonjwa ya Gono
na Kaswende walikuwa 38; kati ya hao, nane walikuwa watoto kati ya miaka 10 na
14.
Habiba
Juma alimaliza darasa la saba katika shule ya msingi kiegei mwaka 1994 na
kusema kuwa, kipindi alichokuwa anasoma yeye hakukuwa na mambo ya ngono kwa
wanafunzi na watu wazima, lakini ilipofika mwaka 1995 ndio mambo ya ngono kwa
wanafunzi yalipoanzia baada ya kuanza kwa machimbo ya madini.
Makwasa Bulenga ni
Afisa elimu wa shule ya msingi wilaya ya Nachingwea alisema kuwa,tatizo kubwa
la wanafunzi kufanya ngono ni kuwepo kwa vibanda vya kuonesha sinema mbalimbali
muda wa usiku.
“Vibanda
vya sinema kwa vijijini ndio tatizo kubwa kwa watoto wa shule ya msingi
kujifunza mambo machafu, huku sinema hizo wakiangalia na watu wazima tena
wanaume hasa wachimbaji wa kutoka sehemu mbalimbali za uchimbaji,”alisema
Bulenga
Bulenga
alisema kuwa ofisi yake imewaita mara kadhaa viongozi wa vitongoji na vijiji
kuwaeleza umuhimu wa vibanda vya sinema kufungwa mapema, lakini juhudi hizo
zimegonga mwamba kwa sababu vibanda hivyo vinaanza kuonesha sinema kuanzia saa
12:00 jioni hadi saa 6:00 usiku na wateja wao wakubwa ni watoto wa shule za
msingi.
Vibanda
vya sinema vinatakiwa kuanza kuonesha sinema saa 8:00 mchana hadi saa 12:00
jioni.
“Sio
tuu kiegei watoto kufanya ngono; na vijiji vingine pia hali ni hiyo hiyo kama
uliyoishudia kiegei, bado tupo katika hali mbaya sana kwa watoto kuanza ngono
mapema kwa wilaya ya Nachingwea,” alisema Bulenga.
Kwa
mujibu wa Bulenga, katika wilaya ya Nachingwea kuna kata 32; kati ya hizo, kata
sita pekee ziko mjini. Nyingine zote ziko vijijini na sehemu kubwa yake ndio
kuna wanafunzi wengi ambao wanafanya ngono baada ya kumaliza kuangalia sinema
za ngono katika maeneo hayo.
Mjini
kuna wanafunzi wapatao 4,789; wavulana ni 2,365 na wasichana 2,424. Vijijini
kuna wanafunzi 27,047; kati yao,
wavulana wako 13,319 na wasichana ni 13,728. Walimu waliopata mafunzo
kuhusu somo la elimu lika kwa wilaya ya Nachingwea wako 23; wanaume 14 na
wanawake9.
Inapaswa
kuwa na walimu ambao wamepatiwa elimu lika 300, ili kiweza kukidhi idadi ya
wanafunzi wa shule za mjini na vijijini katika wilaya ya Nachingwea kwa sasa.
Walimu
ambao hawakupata mafunzo lakini wanafundisha somo hilo la elimu lika wako 200;
wanaume 116 na wanawake 84. Hii inachangia uwajibikaji mdogo kwa walimu ambao
hawajapatiwa mafunzo ya somo hilo jinsi ya kumfundisha mwanafunzi akajiepusha
na ngono.
Kwa
upande wake, Jane Mrema mshauri wa masuala ya jinsia na kutetea haki za
watoto na vijana kutoka Plan International alisema kuwa, tatizo la shule ya
msingi Kiegei kwa watoto kuanza ngono halifahamu.
Mrema
alisema kuwa watoto wanalengwa na shirika la Plan International ni kuanzaia
mwezi mmoja mpaka miaka 18, hasa kwa watoto wa kike pamoja na walemavu. Kwa
sasa wanafanya kazi katika mikoa mitano nayo ni Mwanza, Geita, Morogoro, Pwani
na Dar es salaam lakini pia wanafanya katika wilaya sita ambazo ni Kibaha,
Kisarawe, Kilombero, Sengerema, Ilemela, Geita na Ilala.
“Tunamuelisha
mtoto wa kike kutambua haki yake ya kupata elimu bora na afya bora, pia mtoto
kufahamu unyanyasaji wa kijinsia majumbani na njiani akienda shuleni,
pamoja na kuangalia mazingira ambayo yapo hatarishi kwa kupata unyanyasaji wa
kijinsia kwa mtoto wa kike,” alisema Mrema.
Aidha
Plan International wamejenga mabweni katika wilaya mbalimbali kama Ilala katika
shule ya sekondari sakara, kibaha shule ya sekondari ya ruvu, mwanza na
geita kila bweni linauwezo kuchukua watoto 100, pia wamejanga choo na mabomba
ya maji safi.
Kwa
sasa kuna kampeni nyingine ijulikanayo kama kwa sababu mimi ni msichana
ambayo lizinduliwa mwishoni mwezi wa Octoba mwaka jana, lengo kubwa la kampeni
hii ni, kuhamasisha jamii kutetea haki za mtoto wa kike kwa sababu watoto wa
kike ndio waathirika wakubwa.
Kampeni
hii ilikuwa na ujumbe usemao maisha yangu, haki yangu tokomeza ndoa za utotoni,
kampeni hii hasa inajikita kumtetea mtoto wa kike kuepukana na unyanyasaji wa
kijinsi na kupata haki zake za msingi na elimu bora.
Pia
wamejikita katika suala la afya ya uzazi kwa watoto wa kike, kwa kuwajengea
uwezo kujilinda na kujitunza na kufikia ujana vizuri, pia kutokomeza mira
potofu kama ukeketaji na ndoa za utotoni.
0 comments:
Post a Comment