Thursday, January 10, 2013

TEMBO WANAENDELEA KUUWAWA NACHINGWEA

Baadhi ya mabaki ya mifupa ya mnyama Tembo ambaye alipigwa risasi na majangiri katika msitu wa Nachingwea na kukimbia ovyo kwa maumivu na kwenda kufia katika Kijiji cha Kiegei Kata ya Kiegei Wilaya ya Nachingwea Mkoa wa Lindi, Baadhi ya Wanakijiji walisema kuwa Tembo wanauliwa kila mara katika msitu unaozunguka Kijiji cha Kiegei hadi kuelekea Wilaya ya Liwale, tunaiomba Wizara ya Maliasiri na Utalii kulimulikia macho suala la ujangili katika msitu wa Nachingwea. Hivi karibu kumetokea wimbi la ukamataji wa Meno ya Tembo katika sehemu mbalimbali za Tanzania na Nje ya Nchi.

0 comments:

Post a Comment