Thursday, January 17, 2013

KUTANA NA MLEMAVU ANAYEISHI KWA STAILI YA AINA YAKE

Juma Mpukuta ni Mlemavu wa Viungo kwa muda wa miaka 20 sasa, amepata ulemavu huo baada ya kuumwa miguu kwa miaka saba alivyopona ndio miguu hiyo ikawa haina nguvu ya kukanyaga chini, kwa sasa anatembea kwa kutumia mikono yake miliwi na miguu ikiwa inaburuza chini.

"Nipo hapa katika mlango huu wa kuingia katika Soko la Kimataifa la Samaki Feri kwa muda wa miaka miwili, nalinda ndoo za wafanyabiashara ya samaki wanaoingia sokoni kununua samaki na mahitaji mengine kama mafuta ya kukaangia samaki pamoja na pilili wananilipa kuanzia Tshs. 1000 hadi 2000 kwa ndoo moja kulinda kwa muda wa saa tatu hadi nne, hii ndio kazi yangu inayoniingizia pesa ya chakula na watoto wangu nyumbani, nimeacha kuombaomba katika mitaa mbalimbali kwa miaka miwili sasa na sidhani kama nitaludia kuomba tena maana hapa siku kama nikiwa sipo wafanyabiashara wa samaki wanapata taabu sana ya sehemu ya kutunza ndoo zao za samaki," alisema Juma Mpukuta.

Kazi hiyo ya kutunza mizigo ya wafanyabiashara kwa siku anapata kuanzia Tshs. 5000 hadi 10,000 pesa ambayo inakizi mahitaji yake. Juma anawaomba wafadhili mbalimbali kumsaidia baiskeli ya miguu mitatu ambayo itamsaidia kuwahi katika kibarua hicho cha kulinda mali wa watu pamoja na mwavuli  mkubwa wa kujikinga na mvua na jua, maana kwa sasa anapata shida sana kutembelea mikono na wakati mwengine anapata magonjwa ya kuambukiza kwa kutokana na mazingira anayoshika sio safi.

0 comments:

Post a Comment