Monday, January 21, 2013

SHULE ZA SEKONDARI ZA KATA ZAKUMBWA NA UHABA WA MABWENI MTWARA













Mwajuma Ramadhi ni mwanafunzi wa kidato cha tatu  katika Shule ya Sekondari ya Mkoma iliyoko katika Wilaya ya Newala Mkoa wa Mtwara, anayeishi katika nyumba ya kupanga iliyoko karibu ya shule ambayo anasoma kwa mwezi analipa kodi Tshs 2500. 
Pia Athumani Hamza Mwanafunzi wa Kidato cha pili anayesoma katika shule ya sekondari ya Mnyambe iliyoko katika Wilaya ya Newala, naye anaishi katika nyumba ya kupanga kwa mwezi analipa kodi Tshs. 2000, Shuleni Mnyambe kuna bweni la kulala wanafunzi, lakini mzazi wake hana pesa ya kulipia bweni kwa mwaka Tshs.100,000.

"Nasoma kwa shida sana usiku kwa kutokana na nyumba ninayokaa haina umeme wa solar inanibidi kusoma kwa kutumia kibatali, macho yanauma sana kwa sababu mwanga wa kibatari ni mdogo siwezi kuona vema maandishi, na muda mwengine natumia tochi kama nyumbani hawajanipa pesa ya matumizi ikiwa kununua mafuta ya taa, sio tuu pesa ya kununua mafuta ya taa kwa ajili ya kusomea usiku hata pesa ya matuzi nacheleweshewa kutumiwa nyumbani inanilazimu kufanya kibarua cha kuchota maji kwa kutumia baiskeli na kulima mashamba kama kibarua ili nipate pesa ya kununua chakula, wakati wa kufanya kibarua wenzangu wanaendelea na masomo darasani," alisema Mwajuma.
Pesa ya matumizi kwa mwanafunzi wa Newala ambaye anaishi nje ya shule anatakiwa kupewa Tshs. 50,000 pamoja na unga, sukari, majani ya chai, maharage, dagaa, sabuni na mafuta ya taa kwa miezi miwili.

Kwa sasa Wilaya ya Newala ina shule za Sekondari za Kata zipatazo 28 kati ya hizo shule nne tu ndio zinamabweni ya kulala wanafunzi wakike na wakiume nazo ni Nangwanda, Mtangalanga,Kihuta na Mnyambe.

2 comments:

  1. serikali iangalie hili suala kwan ni hatari sana kwa wanafunz kukaa mitaan...mabweni ni bora kwa usalama wao pamoja na maendeleo yao kitaaluma.

    ReplyDelete
  2. namoneya uruma sana uyo Mtoto wa kike kuna kusoma hapo kweli

    ReplyDelete