Monday, February 4, 2013

LICHA YA KUPUUZWA, MKUNGA WA JADI AZALISHA WANAWAKE 212 KWA MIEZI KUMI


">Na Gordon Kalulunga, Mbeya
“SINA utaalam wa kisasa. Sijawahi kutembelewa na kiongozi wa Hospitali. Lakini jamii inanitambua na kuthamini mchango wangu kwa wajawazito wenye uhitaji wa kujifungua’’
Ndivyo anavyoanza kusema Mkunga Agripina Fredrtick Sikanyika (37) maarufu kwa jina la Mama Namwinji, mkazi wa Kijiji na kata ya Mbuyuni wilayani Chunya mkoani Mbeya alipotembelewa na Mwandishi wa makala haya Octoba, 2012. 

Anasema imemlazimu kuwaachia nyumba yake wagonjwa na wajawazito wanaofika kwa ajili ya kujifungua nyumbani kwake baadhi wakitokea hospitali na zahanati mahala wanakoishi.
Anasema alianza huduma hiyo ya ukunga mwaka 2000 na mwaka 2011 alizalisha wajawazito 114 na mwaka 2012 kwa miezi kumi wajawazito 212 walijifungulia nyumbani kwake hapo.
Ninapomuuliza mahala wanapojifungulia wanawake hao, ananionesha mkeka wa matete maarufu kama Msengele. 

Licha ya wanawake hao kujifungua salama. Anasema wanawake wawili kati ya hao, walijifungua watoto ambao walikuwa na ulemavu wa ajabu.
Anafafanua kuwa mwanamke wa kwanza kujifungua mtoto mwenye ulemavu(kiumbe cha ajabu….), alijifungua Septemba 15,2012 ambapo kichanga hicho kilikuwa na sikio moja, mguu mmoja, mdomo na pua vikiwa vimeungana na alifariki muda mfupi baada ya kujifungua.

‘’Siku iliyofuata yaani Septemba 16,2012 kuna mwanamke ambaye alijifungua mtoto aliyekuwa na kichwa kinachofanana na ndama ya Ng'ombe na kiwiliwili cha binadamu’’ anasema Agripina.
Licha ya kazi hiyo ngumu anayoifanya usiku na mchana na kuishia kupata zawadi ndogo ndogo kutoka kwa wajawazito hao au wenza wao, mkunga huyo wa jadi hana kitanda cha kujifungulia wajawazito, glovu na makaratasi yanayohitajika kwa ajili ya kutandika wakati mjamzito akijifungua. 

Licha ya kutokuwa na elimu ya kisasa juu ya masuala ya afya, Agripina anasema anapompokea mjamzito nyumbani hapo anamuuliza kama alikuwa akihudhuria kliniki na anaangalia kadi zao na baada ya hapo anaandika majina yao na wanakotokea.

“Ninafanya hivyo ili kujua wajawazito hao wanatokea eneo gani na endapo bahati mbaya mjamzito anaweza kupata matatizo makubwa wakati wa kujifungua niweze kuujulisha uongozi wa serikali ya kijiji na kumsafirisha kwa urahisi au kuwajulisha viongozi wa eneo anakotokea’’anasema Agripina. 

Ananionesha daftari lake ambalo anaorodhesha kila mwanamke anayejifungulia hapo na hawa wafuatao ndiyo waliojifungulia kwa mkunga huyo tangu Januari mpaka Octoba, 2012 na tarehe walizojifungua kwenye mabano. 

Theofina Tanesco (1.01.2012), Grace Eneliko(1.01.2012), Sinela Nicolaus(06.01.2012),Justina Enock(13.01.2012),Getruda Nestory(13.01.2012), Paslaalia Vicent(14.01.2012), Devota Alfredy(17.01.2012), Agnes Samson(17.01.2012), Pili Luhende(18.01.2012) Holo Shitungulu(19.01.2012), Asia Luca(20.01.2012), Rehema Uayu(22.01.2012) na Sabina Willium(24.01.2012). 

Eliza Wilson(30.01.2012), Eliza Usinza(4.02.2012), Sabina Roma(9.02.2012), Gindu Sangayende(10.02.2012), Esther Hamis(13.02.2012), Paskalia Vicent (16.02.2012),Ngile Charles(25.02.2012), Holo Tungu(19.02.2012), Neema Christopher(19.02.2012), Lucia Charles(21.02.2012), Agnes Christopher(27.02.2012), Neema Charles(28.02.2012) na Christina Benard 29.02.2012. 

Helena Boniphace(29.02.2012), Jute Luhinza(29.02.2012), Oliva John(29.02.2012), Mary Chambo(01.03.2012), Defloz Adam(01.03.2012), Choyo Shija(02.03.2012), Hoga Charles(06.03.2012), Sumuni Martin(06.03.2012), Shele Uashinje(09.03.2012), Juliana James(10.03.2012), Jelemana Pambano(11.03.2012), Regina Jerad(11.03.2012), Anacleta Helman(14.03.2012), Sai Nosutina(17.03.2012), Yunge Mathias(19.03.2012) na Kwangu Charles(29.03.2012). 

Jumanne Shija(29.03.2012), Sevelina Modat(29.03.2012), Agnes Joseph(13.04.2012), Lega Samson(13.04.2012), Maria Boniphace(13.04.2012),Pastralia Christopher(16.04.2012), Anacleta Edes(16.04.2012), Prica Boniphace(21.04.2012), Yusta George(22.04.2012), Salome Alone(22.04.2012), Joyce Edwin(23.04.2012),Lori Chikono(24.04.2012),Malalina Juma(29.04.2012), Flavia Thobias(29.04.2012) na Getruda Linus(29.04.2012). 

Faustine Paul(29.04.2012), Grace Kasema(30.04.2012), Christina Kisiwani(8.05.2012),Kundi Lutuma(15.05.2012), Lucia Gabriel(18.05.2012), Rehema Andrew(19.05.2012), Nindi Makeja(21,05.2012), Rahab Shija(23.05.2012), Jenipha Stanslaus(27.05.2012), Getruda Frank(29.05.2012), Bohari Abubakar(30.05.2012), Riziki Paulo(2.06.2012), Magreth Joseph(5.06.2012) na Agnes Albeto(06.06.2012). 

Luli Makele(08.06.2012), Mary Thomas(09.06.2012), Suzan Pascal(09.06.2012), Shame Shinge(10.06.2012), Getruda Paul(12.06.2012), Christina Nestory(14.06.2012), Joyce John(22.06.2012),Therezia Anthon(25.06.2012), Frola Roman(30.06.2012),Pundo Sichone(06.07.2012), Venesia Fredrick(9.07.2012), Mwasu Mwandu(11.07.2012),Kwangu Malundeji(14.07.2012), Noelia Boniphace(16.07.2012) na Sophia Frank(17,07.2912). 

Ngane Mahele(21.07.2012), Matrida Shija(28.07.2012), Dotela Nelson(29.07.2012), Mbalu Tutonja(03.08.2012), Winfrida Fedeliko(08.08.2012), Astelia Modeste(19.08.2012),Kulwa Ngassa(20.08.2012),Paskalia White(21.08.2012),Mvud Salum(21.08.2012), Anacleta George(21.08.2012), Monica Kulwa(21,08.2012), Olo Kikono(21,08.2012), Maria Kilanja(22.08.2012), Lucia Mateo(22,08.2012),Milliam Salum(22.08.2012), Anacleta George(2.08.2012) na Shoma Kashinde(23.08.2012),Wembe Tone(23.08.2012),Luli Luwassa(23.08.2012), Mbuke Luhende(23.08.2012), Neema Linus(23.08.2012), Justina Edward (23.08.2012),Mbalu Mele(24.08.2012), Oliva Frank(24.08.2012),Rabi Machia(24.08.2012),Wemelas Landam(24.08.2012) na Olive Nayoni(24.08.2012). 

Sai Mihamba(24.08.2012), Salome Smart(25.08.2012), Tatu Kipunga(25.08.2012), Dodecia Anthon(25.08.2012), Grace Burton(25.08.2012), Asteria Paskalia(25.08.2012), Paulina Simwamba(26.08.2012), Ilambe John(26.08.2012), Rozalia Fredy(26.08.2012),Paulina Moris(26.08.2012), Anacleta James(26.08.2012), Asia Lucas(26.08.2012), Rehema Kaga(27.08.2012),Sabina Willium(27.08.2012) na Minzi Tungua(28.08.2012).

Regina Mandela(28.08.2012), Selina Samson(28.08.2012), Holo Mayunga(28.08.2012), Mage Ismail(29.08.2012), Lucia George(29.08.2012), Auleria Kenneth(29.08.2012), Zuwanda Njule(29.08.2012), Edna Robi(31.08.2012),Maclina William(31.08.2012), Maria Laulent(31.08.2012), Winfrida Ezekiel(31.08.2012), Winfrida Linus(01.09.2012), Esther James(01.09.2012), Telezia Samson(01.09.2012),Kulwa Maliga(2.09.2012), Hamba Kilindilo(03.09.2012), Magreth Masanja(3.09.2012) na Therezia Zambi (03.09.2012). 

Clemencia Langson(14.09.2012), Olonica Huzuni(15.09.2012),(Shiji Paulo(16.09.2012), Wilfrida Mbawe(17.09.2012), Amina Silungwe(18.09.2012), Justa Aliliado(18.09.2012),Paskalia Mitodu(18.09.2012), Sharifa Clestusi(19.09.2012), Sara Kani(20.09.2012), Win Songeti(21.09.2012), Justina George(21.09.2012),Paskalia Killian(21.09.2012), Mbuke Masile(22.09.2012), Tabu Donat(22.09.2012), Kwangu Mchele(23.09.2012) na Prisca Odelasi(23.09.2012). 

Zowe Isasi(23.09.2012), Win Songole(24.09.2012),Beaty Albeto(24.09.2012), Kabula Luwinza(24.09.2012), Anacleta Patson(24.09.2012), Anacleta Mitod(24.09.2012),Kalista Cosmas(25.09.2012), Giadu Joseph(25.09.2012), Defloza James(25.09.2012), Jane Mahuna(25.09.2012), Juke Samwel(29.09.2012), Mbalu Charle(30.09.2012),Lucia Ostat(30.09.2012), Melina Elias(01.10.2012) na Maltina John(01.10.2012). 

LuminataUgata(01.10.2012), Lenancia Paskali(01.10.2012), Asteria Blazio(02.10.2012), Mbala Lagola(02.10.2012), Jenipha Michael(02.10.2012), Maria Leonard(02.10.2012), Gugwe Joseph(03.10.2012),Anastazia Mwali(03.10.2012), Tatu Said(03.10.2012),Prisca Vicent(03.10.2012), Sephania Amin(03.10.2012), Anastazia Chrisphin(03.10.2012), Agnes Alex(04.10.2012),Esther Mwazi(04.10.2012) na Wende Njuli(04.10.2012). 

Pascalia Aloyce(05.10.2012), Devetalia Julius(05.10.2012), Rosemary Sanzu(05.10.2012), Safina Adam(05.10.2012), Marieta Fransisco(06.10.2012), Mbahi Machia(06.10.2012),Kunde Shija(06.10.2012),Shani Charles(06.10.2012), Pendo Charles(06.10.2012), Wande Lugombe(07.10.2012),Kambi Kashinje(07.10.2012) na Jenipher Isack(07.10.2012).
Julieta Philipo(07.10.2012),Kashinje Luhande(08.10.2012), Nolia Maiko(08.10.2012),Lucia Satiel(08.10.2012), Sabina Elias(08.10.2012),Zuhura Daud(09.10.2012), Jenipher Alphonce(09.10.2012) na Kundi Lugola(09.10.2012). 

Afisa Mtendaji wa Kijiji hicho cha Mbuyuni Konrad Umboka, anasema Serikali ya Kijiji imeridhia Mkunga huyo kutoa huduma za uzazi na kwamba wao kama Serikali wanamtembelea na kumpatia elimu ya usafi wa mazingira. 

‘’Natoa wito kwa serikali hasa wizara ya afya kumsaidia mkunga huyu maana amekuwa msaada mkubwa kwa wanawake hapa kijijini na wanaotoka maeneo mbalimbali ya Tanzania’’ anasema Umboka.
Mwenyekiti wa chama cha waganga na wakunga wa jadi (CHAWATIATA) kata ya Mbuyuni Bruno Mbegeze anasema chama hicho kinamtambua na kuthamini kazi zake za kuzalisha wanawake na kutibu magonjwa mengine. 

‘’Wito wangu kwa Serikali kama itaona umuhimu wa huduma anayoitoa mkunga huyu kama tunavyoona wananchi basi imwongezee nyenzo za kutendea kazi ikiwemo elimu ya kujikinga na maabukizi ya VVU’’ anasema Mbegeze.

Mratibu wa huduma za Afya ya uzazi na mtoto mkoa wa Mbeya Prisca Butuyuyu, anasema kuwa anatambua kuwa mkunga huyo anatoa huduma ya kuzalisha lakini kitengo chake kiliwahi kumkataza na haelewi kwanini anaendelea kutoa huduma hiyo.

0 comments:

Post a Comment