Monday, March 18, 2013

UKOSEFU WA MAJI SAFI BUNDA WAPELEKEA WANANCHI KUTUMIA MAJI MACHAFU YA MITARO

 
Wakazi wa wilaya ya Bunda  mkoa wa Mara, wapo hatarini kupata magonjwa ya mlipuko katika kipindi hiki cha mvua, yanayosababisha na ukosefu wa maji safi na salama.

Tatizo la ukosefu wa maji safi na salama katika wilaya hiyo, ni la zaidi ya miaka 20 wakazi hao wanatumia maji ya katika marambo yanayopatikana baada ya kunyesha mvua na maji katika mifereji ya maji machafu.
Maji-shida
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Joseph Marimbe alisema kuwa, tatizo la maji kwa Bunda ni la miaka zaidi ya 20, na kusababisha wananchi wanapata magonjwa mbalimbali ya mlipuko  kwa kukosa maji safi na salama.
"Tatizo la maji lipo tena kubwa sana hapa Bunda, maana miundombinu ya maji kama mabomba yalijengwa mwaka 1970, kipindi hicho kulikuwa na wakazi wapatao 70,000 lakini kwa sasa kuna wakazi wapatao 400,000 na bado wanatumia miundombinu ileile ya maji ya miaka 70,"alisema Marimbe.
Aidha alisema kuwa kwa sasa ndio wameanza kujenga miundombinu mipya ya maji kama mabomba na mateki, mradi huo ukikamilika utagharimu shillingi Bilioni 30, unafadhiliwa na Bank ya Afrika, Bank ya Dunia na Serikali ya Tanzania.
Marimbe alisema kuwa mradi huo wa maji ukikamilika utadumu kwa zaidi ya miaka 20, kwa wakazi hao kupata maji safi na salama na kupunguza magonjwa mbalimbali ya mlipuko kama kipindupindu na kuhara, lakini yeye kama Mwenyekiti wa Halmashauri hafahamu mradi huo utakamilika mwaka gani.
Joseph-Marimbe
Joseph Marimbe, Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya Bunda akifafanua juu ya tatizo sugu la maji kwa zaidi ya miaka 20
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa wilaya hiyo Dokta Rainer Kapinga alisema kuwa, tatizo la magonjwa ya mlipuko kwa Bunda ni kubwa kwa kutokana na kukosa maji safi na salama.

Dokta Kapinga alisema kuwa mwaka 2010 kulikuwa na kambi za kipindupindu zaidi ya saba, na wagonjwa wapatao 97 kati ya hao wagonjwa 13 walipoteza maisha kwa kuugua ugonjwa huo.

"Kwa sasa bado hatujapata tatizo la kipindupindu ila kuna tatizo sugu la ugonjwa wa Mkojo Mchafu U.T.I, Kuhara na ugonjwa wa Ngozi kwa sababu ya matumizi ya maji machafu wanayojichotea ovyo wakazi mbalimbali wa Bunda," alisema Dokta Kapinga.

Aidha alisema kuwa katika magonjwa kumi yanayoitesa wilaya hiyo, magonjwa manne yanatokana na matumizi ya maji machafu, wanayotumia wakazi wa hapa, magonjwa hayo ni Malaria, Kifua, Kichomi, Kuhara, Kipindupindu, ugonjwa wa Ngozi, U.T.I, magonjwa zinaa kama Kisonono, maambukizi ya Gono, Kaswende na UKIMWI.

Kutoka katika kata ya Guta kulikokuwa na Ziwa Victoria mpaka kufika Bunda mjini ni kilometa 15 tu, kwa nini wilaya hiyo inatatizo la maji kwa miaka zaidi ya 20, dumu la maji linauzwa kuanzia sh. 200 hadi sh. 500, wakati maji ya ziwa yapo umbali wa kilometa 15? huu ni uzembe wa watawala katika wilaya hiyo.

0 comments:

Post a Comment