Tuesday, March 5, 2013

MASIKINI MGANGA MKUU HANA CHOO

Chooo cha waganga katika kituo cha afya cha Ikizu wilaya ya Bunda mkoa wa Mara kimetitia chini ya aridhi, choo hiki kilikuwa kinatumika na nyumba mbili za waganga katika kituo hicho, kwa sasa inawalazimu familia hizo kutumia choo kimoja na wagonjwa wanaofika kutibiwa katika kituo hicho ambacho kipo zaidi ya mita 150, hali hiyo inaweza kusababisha magonjwa mbalimbali ya kuambukiza.

Ni zaidi ya miezi mitano sasa toka choo hicho kititie aridhini na hakuna jitihada zozote za makusudi kuweza kujenga choo kingine kwa watumishi hao, kwa hali hii je watoa huduma wa kituo hiki wanaweza kufanya kazi ya kutoa huduma kiukamilifu!

0 comments:

Post a Comment