Wednesday, April 17, 2013

NAPENDA KUSOMA

Watoto Diana Joseph (2) Tarik Faraji (2), wakijifundisha kusoma katika karasi lililoandikwa pamoja na kuchorwa katuni mbalimbali. Watoto hawa waliokuwa wanajifundisha kusoma baada ya kumaliza kupima uzito na kupatiwa dawa ya minyoo katika kituo cha kupima watoto kwa mwezi mara moja kupitia gari maalumu la Bank ya NBC. 

Kituo hicho kipo Goba Umoja Manispaa ya Kinondoni mkoa wa Dar es Salaam. Sababu kubwa ya kuwa na vitu hivi ni kutokana na eneo hili kuwa mbali na zahati ya Goba, kwa hiyo inakuwa ngumu kwa akinamama kuwapeleka kupima watoto kila mwezi. Kituo hicho kimewapima watoto wa chini ya miaka 5 wapatao 50 kwa siku ya leo.

0 comments:

Post a Comment