Mama

Nani kama Mama .

Afya ya Mimba

Mwanamke anayetaka kubeba mimba anashauriwa aache kunywa pombe na kuvuta sigara.

Mama na Mtoto

Mazingira mazuri ya Afya ni Moja ya njia ya kuepuka matatizo ya mama wakati wa kujifungua.

Tuwalinde watoto

watoto 200 kati ya 100,000 wanapoteza maisha wakati wa kuzaliwa na baada ya kuzaliwa, idadi hii ya vifo ni kubwa sana hapa nchini Tanzania.

Karibu kwenye blog hii kwa Habari za Afya ya Mama na Mtoto.

Kufikia mwaka 2010, takwimu zilikuwa zinaonesha kwamba kila wanawake 454 katika vizazi hai 100,000 walikuwa wanapoteza maisha wakati wa ujauzito au kujifungua kwa matatizo mbalimbali ya uzazi.

watoto 200 kati ya 100,000 wanapoteza maisha wakati wa kuzaliwa na baada ya kuzaliwa, idadi hii ya vifo ni kubwa sana hapa nchini Tanzania..

Friday, January 18, 2013

MAJI YAWA DHAHABU RUFIJI

Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Mlanzi katika Wilaya ya Rufiji Mkoa wa Pwani, wakichota maji ya matuzi ya kila siku ya nyumbani kwa shida sana katika kisima kiferu, kwa muda mrefu upatikaji wa maji salama katika kijiji hicho umekuwa wa shida sana, mpaka inawalizimu akinamama na watoto kushinda na kukesha usiku kisimani hapo kusubiri maji.

"Maji ni dhahabu hapa kijijini kwetu nimefika toka saa 5 hasubuhi mpaka sasa saa 10 bado sijapata maji hata ndoo moja na nyumbani nimecha pakavu hakuna maji hata tone, kama kunatokea mtoto anaharisha au mimi mwenyewe sina maji ya kumpa kijisafisha au kumeza dawa, ukifika hapa kisimani unatakiwa kuacha kazi zingine zote usubiri mpaka utakapo pata maji, unasubiri kwa saa tatu unachota ndoo mbili yamekuwa yameisha kisimani unasubiri tena baada ya saa tatu unachota ndoo mbili, tunatumia muda mwingi sana kusubiri maji badala ya kufanyashughuli zingine za kimaendeleo kama kulima na kipindi hiki ndio cha kilimo lakini mashamba yamejaa majani akinamama tuko busy kusubiri maji kisimani," alisema Maimuna Mkima.

Wakazi wa Kijiji hicho wanaiomba Wizara ya Maji na Umwagiliaji kuwachimbia kisima kirefu cha kisasa ili wapate maji kiurahisi na kuondokana na adha ya kushinda na kukesha kisimani kila siku, badala ya kuangalia maendeleo ya kilimo katika mashamba yao.

Thursday, January 17, 2013

KUTANA NA MLEMAVU ANAYEISHI KWA STAILI YA AINA YAKE

Juma Mpukuta ni Mlemavu wa Viungo kwa muda wa miaka 20 sasa, amepata ulemavu huo baada ya kuumwa miguu kwa miaka saba alivyopona ndio miguu hiyo ikawa haina nguvu ya kukanyaga chini, kwa sasa anatembea kwa kutumia mikono yake miliwi na miguu ikiwa inaburuza chini.

"Nipo hapa katika mlango huu wa kuingia katika Soko la Kimataifa la Samaki Feri kwa muda wa miaka miwili, nalinda ndoo za wafanyabiashara ya samaki wanaoingia sokoni kununua samaki na mahitaji mengine kama mafuta ya kukaangia samaki pamoja na pilili wananilipa kuanzia Tshs. 1000 hadi 2000 kwa ndoo moja kulinda kwa muda wa saa tatu hadi nne, hii ndio kazi yangu inayoniingizia pesa ya chakula na watoto wangu nyumbani, nimeacha kuombaomba katika mitaa mbalimbali kwa miaka miwili sasa na sidhani kama nitaludia kuomba tena maana hapa siku kama nikiwa sipo wafanyabiashara wa samaki wanapata taabu sana ya sehemu ya kutunza ndoo zao za samaki," alisema Juma Mpukuta.

Kazi hiyo ya kutunza mizigo ya wafanyabiashara kwa siku anapata kuanzia Tshs. 5000 hadi 10,000 pesa ambayo inakizi mahitaji yake. Juma anawaomba wafadhili mbalimbali kumsaidia baiskeli ya miguu mitatu ambayo itamsaidia kuwahi katika kibarua hicho cha kulinda mali wa watu pamoja na mwavuli  mkubwa wa kujikinga na mvua na jua, maana kwa sasa anapata shida sana kutembelea mikono na wakati mwengine anapata magonjwa ya kuambukiza kwa kutokana na mazingira anayoshika sio safi.

Wednesday, January 16, 2013

SAMAKI PWEZA SIO TU KUTABILI MECHI ZA MPIRA WA MIGUU AFRIKA NA ULAYA? BALI ANALETA KHESHIMA NDANI YA NDOA


"Licha ya kutabili mechi mbalimbali za mpira wa miguu katika Bara la Afrika na Ulaya lakini, ukitumia supu ya samaki pweza inaludisha kheshima ndani ya ndoa, kwa kunywa supu hiyo na mkia wake iliyopikwa vema kwa dakika 30 na kuwekwa viungo vya kukata shombo kama ndimu na tangawizi, ukinywa hiyo baada ya saa moja mambo safi ndani ya ndoa," alisema Mfaume Namkopi mpika na mkaanga pweza wa sokoni feri kwa miaka 21 sasa.
Victar Mwandike ni Afisa Uvuvi wa Sokoni hapo alisema kuwa samaki jamii ya Kamba, Kitaa na Pweza wanaongeza vitamini A katika mwili wa binadmu na huleta kheshima katika tendo la ndoa, samaki pweza akiwa mkubwa kuanzia kilo 8 hadi 9 na akikaa vema kitika mwamba anaweza kumuuwa mvuvi wa pweza kwa kumtumbukiza mikia yake sita puani, masikioni,mdomoni na machoni, mvuvi akiwa hana vifaa vya kujikinga anapoteza maisha. Pweza anakuwa mkubwa mpaka kufikia kilo 50 hadi 60 akiwa ndani ya maji na anapenda kuishi chini ya mwamba.
Mfaume Namkopi mpikaji na mkaangaji Samaki aina ya Pweza katika Soko la Kimataifa la Samaki Feri Jijini Dar es salaam, kazi ya kutengeneza pweza inamnufaisha yeye na familia yake, kwa siku anachemsha na kukaanga zaidi ya sahani 20, kila sahani analipwa Tshs. 2000. Msingi wake ni Tshs. 100,000 kwa kununua mzigo wa kuni na mafuta ya kukangia pweza, kwa mwezi analipa kodi ya sehemu ya kukaangia pweza ni Tshs. 15,000.Hajawahi kunywa maziwa hata mara moja kwa kazi hiyo ya kukaa jikoni kwa muda mrefu, kwa siku anapata Tshs 10000 hadi Tshs. 20000 pesa inayokizi mahitaji yake.
Kwa sasa kilo moja ya samaki pweza inauzwa Tshs. 6,000 kwa pweza wakubwa na kwa pweza wadogo kilo moja ni Tshs. 4,000.

Tuesday, January 15, 2013

HII NI HATARI KWA WALAJI WA SAMAKI

Msaidizi wa Mvuvi akiburuza samaki aina ya kitaa katika Soko la Feri Jijini Dar es salaam, uburuzaji wa samaki kwa aina hii ni hatari sana kwa afya za binadamu. Afisa Afya wa Sokoni Feri Kesia Bernard alisema kuwa uchuuzi wa samaki kwa kuburuza sehemu ambayo sio safi na salama ni kinyume cha sheria na utaratibu wa kubeba samaki hapa sokoni, mvuvi akikamatwa anafanya kitendo hicho anatozwa faini ya Tshs. 10,000 hadi 50,000.Kwa siku tunawakamata wavuvi kuanzi watano hadi saba wanaofanya uchuuzi wa samaki kwa kuwaburuza chini.
Meneja wa Soko hilo la Feri Charles Kapongo alisema kuwa tatizo la ubebaji wa samaki bila ya kufuata taratibu na sheria za soko la samaki zimekithiri hapa sokoni, hii inatokana na wadau wa samaki kukaidi kubeba samaki hao katika vikapu lakini pia ukosefu wa matoroli maalumu ya kubebea samaki kwa muda wa miaka 9 sasa ndio sababu kubwa ya kukithiri kwa uburuzaji wa samaki.
"Tunaiomba Halmashauri ya Wilaya ya Ilala kutununulia matoroli maalumu ya kubebea samaki ili samaki achukuliwe katika mazingira safi na salama,".
Mahitaji ya toroli kwa sasa ni 20 hadi 25, apo awali toroli hizo zilikuwa zinakodishwa kwa siku ni Tshs. 300.

AJIRA KWA WATOTO NCHINI TANZANIA BADO NI TATIZO SUGU

Watoto hawa niliowakuta katika Kijiji cha Mlanzi Wilaya ya Rufiji Mkoa wa Pwani, wakiwa wamebeba ndoo na madumu ya maji kwenye baiskeli, kazi hiyo ya kubeba maji kwa kutumia baiskeli wanalipwa kwa ndoo moja Tsh. 200.
"Shule imefunguliwa tarehe 14 January lakaini mpaka sasa sijaenda kwa sababu ya sina sare ya shule, viatu na madaftari mama ajaninunuria, nafanya kazi ya kuwachotea wanakijiji maji kwa ndoo Tshs. 200 mpaka nipate pesa ya kutosha kununua yunifomu za shule, viatu na madaftari," walisema watoto hao. Bei ya sare za shule kwa sasa ni kuanzi Tshs. 10,000 hadi Tshs.13,000, daftari linauzwa kuanzi Tshs. 500 hadi Tshs 3000.
Kwa siku amepata pesa nyingi ni Tshs. 2000 atauza maji mpaka lini ili apate pesa ya kununua vifaa vya shule? Mzazi wajibu wake ni upi kwa mtoto kama huyu? kuwa na aina hii ya wazazi je utumikishwaji wa watoto utaisha hapa nchini? Kijiji cha Mlanzi kinauhaba wa maji safi na salama, wakazi wengi hasa wanawake hutumia muda mwingi kusubiri maji kisimani.

Saturday, January 12, 2013

MTU NI AFYA IKIWA PAMOJA NA KUJISAIDIA SEHEMU SAFI SIO VICHAKANI

Baadhi ya Abiri wa kwenda Mikoa ya Songea, Mbeya, Mwanza na Bukoba wakipata huduma ya choo katika eneo la Mkambalani Wilaya ya Morogoro katika Mkoa wa Morogoro. Huduma hii ya choo ni salama kwa wasafiri mbalimbali kujisaidia wakiwa njiani, kwa sababu kuna maji ambayo watatumia kujisafisha baada ya kujisaidia, pia inawakinga na magonjwa mbalimbali ya kuambukiza kwa abiria kujisaidia katika vichaka ambavyo mabasi husimama kwa pamoja katika eneo moja na abiria hushuka kujisaidia bila hata ya kuwa na maji ya kujisafisha.
Sehemu kubwa ya barabara za kwenda mikoani mbalimbali hapa nchini Tanzania, hakuna huduma ya choo abiria wengi hulazimika kujisaidia katika vichaka mbalimbali, sio tu kuhatarisha afya zao bali ni uchafuzi wa mazingira kwa kujisaidia sehemu ambayo sio rasmi kwa huduma hiyo.

MAANDALIZI YA SHULE YA PAMBA MOTO JIJINI DAR

Baadhi ya Wakazi wa Jijini Dar es salaam, wakinunua vifaa mbalimbali vya shule katika Soko la Mchikichini Wilaya ya Ilala Mkoani Dar, Wakazi hao wamelalamika kupande kwa bei kwa vifaa hivyo, kiatu cheusi cha mtumba kwa mtoto wa darasa la pili kinauzwa kuanzi Tsh. 20,000 hadi Tsh.30,000, Mwaka jana kiatu kama hicho kilikuwa kinauzwa Tshs. 10,000 hadi Tshs.15,000. Wafanyabiashara walio wengi katika soko hilo ni vijana ambao wameacha utumiaji wa madawa ya kulevya na uporaji na kuamua kujiajiri wenyewe.
"Nimeanza biashara ya kuuza viatu vya aina mbalimbali kwa muda wa miaka 3 sasa, biashara ni nzuri napata pesa ya kujikimu na familia yangu, kabla ya kuja hapa sokoni mchikichini nilikuwa mtaani tuu nakabakaba watu huko kwetu Masasi Mtwara, lakini kwa sasa nimeacha ukabaji kwa sababu napata pesa ya kutosha katika biashara ya kuuza viatu, kwa siku napata mpaka Tshs. 80,000 biashara ikiwa nzuri kama biashara mbaya napa Tshs.30,000 kwa siku," alisema Salumu Manzi.

Thursday, January 10, 2013

WAKULIMA WA KOROSHO KIJIJI CHA CHIMBENDENGA NACHINGWEA

Baadhi ya wakulima wa korosho katika Kijiji cha Chimbendenga katika Wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi, wakipima korosho zao ghalani kwa mkopo pesa ambayo mpaka sasa bado hawajalipwa.

MKULIMA WA KOROSHO KIJIJI CHA MTUA NACHINGWEA

Halima Chinguile akiwa na baadhi ya magunia na viroba vilivyojazwa korosho katika Kijiji cha Mtua Wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi.Wakulima wa Korosho Nachingwea bado hawajalipwa pesa walizokopesha korosho ghalani mpaka sasa.