Mama

Nani kama Mama .

Afya ya Mimba

Mwanamke anayetaka kubeba mimba anashauriwa aache kunywa pombe na kuvuta sigara.

Mama na Mtoto

Mazingira mazuri ya Afya ni Moja ya njia ya kuepuka matatizo ya mama wakati wa kujifungua.

Tuwalinde watoto

watoto 200 kati ya 100,000 wanapoteza maisha wakati wa kuzaliwa na baada ya kuzaliwa, idadi hii ya vifo ni kubwa sana hapa nchini Tanzania.

Karibu kwenye blog hii kwa Habari za Afya ya Mama na Mtoto.

Kufikia mwaka 2010, takwimu zilikuwa zinaonesha kwamba kila wanawake 454 katika vizazi hai 100,000 walikuwa wanapoteza maisha wakati wa ujauzito au kujifungua kwa matatizo mbalimbali ya uzazi.

watoto 200 kati ya 100,000 wanapoteza maisha wakati wa kuzaliwa na baada ya kuzaliwa, idadi hii ya vifo ni kubwa sana hapa nchini Tanzania..

Monday, March 4, 2013

HII NDIO BENDERA YA TAIFA

Bendera ya Taifa ikiwa imechanika katika wilaya ya Bunda mkoa wa Mara, Jimboni kwa Wasira.

Sunday, March 3, 2013

MALARIA INAVOMALIZA WATOTO BUNDA

Mwajuma Ramadhani mtoto wa miaka miwili na mwezi mmoja akiwa katika hali mbaya kwa kuumwa ugonjwa Malaria, Winifrida Chales mama wa Mwajuma akiwa amemkamata huku Dokta Msimu Michel akijitahidi kumpima mtoto huyo katika kituo cha afya cha Manyamanyama wilaya ya Bunda mkoa wa Mara,Ugonjwa wa Malaria ni tishio kwa watoto mbalimbali katika wilaya hiyo, asilimia 42 ya watoto wote wanaofikishwa katika zahanati, kituo cha afya na hospitali katika wilaya hiyo wanaumwa malaria ila dawa za kutibu  ugonjwa huo mpaka sasa hazipo katika wilaya hiyo.

Thursday, February 28, 2013

RAHA ILIOJE KUANGALIA KICHANGA

Malaika huyu ana saa mbili tu baada ya kuzaliwa na  Nyangeta Chacha (29) katika hospitali ya mkoa wa Mara, mtoto ana uzito wa  kilo 3 mama wa mtoto anaishi mtaa wa nyakato katika wilaya ya Musoma mjini mkoa wa Mara. Hospitali hiyo imejengwa mwaka 1932 na kuanza kazi kama kituo cha afya mwaka 1933, lakini kwa sasa inakabiliwa na upungufu wa wauguzi mahitaji ni wauguzi 200.

HUU NDIO USAFIRI WA MJAMZITO BUTIAMA

Dereva Bajaji Malegesi Malegesi  akiwa kazini katika kijiji cha Rwamkoma akitokea Butiama Mjini, usafiri huo kwa abiria analipa nauli ya sh. 15,00 lakini kwa mjamzito akikodi analipa sh. 15,000 kutoka Rwamkoma mpaka katika hospitali ya wilaya ya Butiama mkoa wa Mara.

Usafiri huo sio salama kwa wajawazito katika kijiji hicho chenye wakazi zaidi ya 5000 na kila mwezi wanapokea wajawazito kuanzi 10 hadi 15 ambao wanamatatizo ya uzazi na wanahitaji usafiri wa kwenda hospitali.

Wednesday, February 27, 2013

MATATIZO YA HUDUMA ZA AFYA NCHINI TANZANIA

Baadhi ya wajawazito wakisubili huduma katika kituo cha afya cha Manyamanya wilaya ya Bunda, lakini mtoto wa miezi saba akipimwa uzito katika mzani wa kichanga katika zahanati ya Rwamkoma wilaya ya Butiama mkoa Mara.

Monday, February 25, 2013

UTAPIAMLO BADO UPO TANZANIA?

Wakati jamii mbalimbali wakifikiri kwamba ugonjwa wa Utapiamlo umeisha lakini katika Jimbo la Mwibara wilaya Bunda mkoa wa Mara katika kata ya Kibara na Kisori ugonjwa huo bado upo.
Sababu kubwa ya kuwa na ugonjwa huo ni ukame kwa kukosa mvua za kutosha pamoja na kupungua kwa samaki na dagaa katika ziwa Victoria na wanaovuliwa wanaishia kwenye viwanda vya samaki kwa kutengeneza minofu na kusafirishwa nchi mbalimbali.

Watoto hao wangekula samaki na dagaa kwa wingi wangeweza kupata madini ya chuma na protini kwa wingi na ingeweza kupunguza ugonjwa huo.
Kati ya watoto 17,570 watoto 294 wanaumwa ugonjwa wa utapiamlo ambayo ni sawa na asilimia 1.5.

Sunday, February 24, 2013

HUYU NDIO WANAMKE SHUJAA?

Boke Makori ni wifi yake na Nyangeta Maiga Makori wakazi wa kijiji cha Nyambono wilaya ya Musoma vijijini, Boke ndiye 'WANAMKE SHUJAA' aliyemshawishi kaka yake Mwita Makori kuuza ng'ombe ili wapate nauli ya kumpeleka wifi yake kituo cha afya Manyamanyama Bunda ili ajifungue katika uwangalizi wa wataalamu.

"Wifi akiwa na ujauzito wa miezi nane nilianza kumshawishi kaka kuuza japo ng'ombe mmoja ili tupate nauli ya kumpeleka wifi kituo cha afya alikataa kwa mara ya kwanza, lakini sikuchoka kumwambia kila ninapokwenda kumuona wifi maendeleo yake, niliendelea kumwambia zaidi ya mara tano ndio alikubali kipindi hicho Nyangeta alikuwa na ujauzito wa miezi tisa,"alisema Boke

Kwa upande wake mume wake Nyangeta Bwana Mwita Makori alisema ni kweli dada alikuwa akinihiza kuuza ng'ombe mmoja ili apate nauli ya kumpeleka mke wangu kujifungua katika kituo cha afya, nilikubali kwa shingo upande kwa sababu dada amening'ang'aniza kuuza ng'ombe, nilichaguoa kang'ombe kadogo nikauza kwa Tshs. 15,0000.


"Sasa nimeona umuhimu wa kuuza kang'ombe kangu kadogo ili mke wangu apate nauli ya kwenda kituo cha afya, amejifungua vema watoto mapacha ndio nimefika kumchukua kumrudisha nyumbani Musoma vijijini, nawashauri wanaume wa mkoa wa Mara kuwatunza wajawazito na kuwapeleka katika kituo cha afya kujifungua sio kung'ang'ania wakezao kujifungua kwa wakunga wa jadi,"alisema Mwita

Dereva wa Bodaboda Chacha alisema kuwa nasikia fahari kubwa sana kumbeba mama mwenye watoto mapacha kumrudisha kijijini, nitaendesha pikipiki pole pole na kukwepa mashimo ili mama na watoto wafike salama.

Ghalama za kukodi pikipiki kutoka kijijini Nyambono mpaka Bunda ni Tshs. 60,000 kwenda na kurudi kijijini, ni wanawake wangapi wanaowashawishi kaka zao vijijini kuuza ng'ombe, mbuzi,kuku pamoja na mazao ya kilimo ili ipatikane nauli ya kumpeleka mjamzito pindi anapoumwa uchungu kituo cha afya au hospitali?

Ni wanaume wangapi wanaokubali kuuza rasilimali ili mkewe ajifungulie katika kituo cha afya kwa uwangalizi wa wataalamu? kumbe inawezeka kupunguza vifo vya akinamama kwa jamii kubadilika kwa kutoa msaada kwa mjamzito akikalibia kujifungua?

Safari ya kuelekea kijijini ndio hiyooo imeanza kwa familia ya Makori? nadhani atawatunza vema watoto hao mapacha aliowapata ili wawe viongozi  wa baadae katika nchi yetu ya Tanzania.

HII NDIO MATVILLA BEACH NDANI YA MUSOMA

Hii ndio Matvilla Beach iliyoko Musoma Mjini pembeni mwa Ziwa Victoria Mkoa wa Mara.

Friday, February 22, 2013

AJIRA KWA MTOTO BADO KITENDAWILI KISICHOPATIWA JIBU?

Saa 4:00 asubuhi muda wa shule mtoto anachunga ng'ombe na mbuzi katika kijiji cha Mugundu wilaya Iramba mkoa wa Singida, nani atalimaliza hili?