Mama

Nani kama Mama .

Afya ya Mimba

Mwanamke anayetaka kubeba mimba anashauriwa aache kunywa pombe na kuvuta sigara.

Mama na Mtoto

Mazingira mazuri ya Afya ni Moja ya njia ya kuepuka matatizo ya mama wakati wa kujifungua.

Tuwalinde watoto

watoto 200 kati ya 100,000 wanapoteza maisha wakati wa kuzaliwa na baada ya kuzaliwa, idadi hii ya vifo ni kubwa sana hapa nchini Tanzania.

Karibu kwenye blog hii kwa Habari za Afya ya Mama na Mtoto.

Kufikia mwaka 2010, takwimu zilikuwa zinaonesha kwamba kila wanawake 454 katika vizazi hai 100,000 walikuwa wanapoteza maisha wakati wa ujauzito au kujifungua kwa matatizo mbalimbali ya uzazi.

watoto 200 kati ya 100,000 wanapoteza maisha wakati wa kuzaliwa na baada ya kuzaliwa, idadi hii ya vifo ni kubwa sana hapa nchini Tanzania..

Thursday, February 28, 2013

RAHA ILIOJE KUANGALIA KICHANGA

Malaika huyu ana saa mbili tu baada ya kuzaliwa na  Nyangeta Chacha (29) katika hospitali ya mkoa wa Mara, mtoto ana uzito wa  kilo 3 mama wa mtoto anaishi mtaa wa nyakato katika wilaya ya Musoma mjini mkoa wa Mara. Hospitali hiyo imejengwa mwaka 1932 na kuanza kazi kama kituo cha afya mwaka 1933, lakini kwa sasa inakabiliwa na upungufu wa wauguzi mahitaji ni wauguzi 2...

HUU NDIO USAFIRI WA MJAMZITO BUTIAMA

Dereva Bajaji Malegesi Malegesi  akiwa kazini katika kijiji cha Rwamkoma akitokea Butiama Mjini, usafiri huo kwa abiria analipa nauli ya sh. 15,00 lakini kwa mjamzito akikodi analipa sh. 15,000 kutoka Rwamkoma mpaka katika hospitali ya wilaya ya Butiama mkoa wa Mara. Usafiri huo sio salama kwa wajawazito katika kijiji hicho chenye wakazi zaidi ya 5000 na kila mwezi wanapokea wajawazito kuanzi 10 hadi 15 ambao wanamatatizo ya uzazi...

Wednesday, February 27, 2013

MATATIZO YA HUDUMA ZA AFYA NCHINI TANZANIA

Baadhi ya wajawazito wakisubili huduma katika kituo cha afya cha Manyamanya wilaya ya Bunda, lakini mtoto wa miezi saba akipimwa uzito katika mzani wa kichanga katika zahanati ya Rwamkoma wilaya ya Butiama mkoa Mara....

Monday, February 25, 2013

UTAPIAMLO BADO UPO TANZANIA?

Wakati jamii mbalimbali wakifikiri kwamba ugonjwa wa Utapiamlo umeisha lakini katika Jimbo la Mwibara wilaya Bunda mkoa wa Mara katika kata ya Kibara na Kisori ugonjwa huo bado upo. Sababu kubwa ya kuwa na ugonjwa huo ni ukame kwa kukosa mvua za kutosha pamoja na kupungua kwa samaki na dagaa katika ziwa Victoria na wanaovuliwa wanaishia kwenye viwanda vya samaki kwa kutengeneza minofu na kusafirishwa nchi mbalimbali. Watoto hao wangekula...

Sunday, February 24, 2013

HUYU NDIO WANAMKE SHUJAA?

Boke Makori ni wifi yake na Nyangeta Maiga Makori wakazi wa kijiji cha Nyambono wilaya ya Musoma vijijini, Boke ndiye 'WANAMKE SHUJAA' aliyemshawishi kaka yake Mwita Makori kuuza ng'ombe ili wapate nauli ya kumpeleka wifi yake kituo cha afya Manyamanyama Bunda ili ajifungue katika uwangalizi wa wataalamu. "Wifi akiwa na ujauzito wa miezi nane nilianza kumshawishi kaka kuuza japo ng'ombe mmoja ili tupate nauli ya kumpeleka wifi kituo cha...

HII NDIO MATVILLA BEACH NDANI YA MUSOMA

Hii ndio Matvilla Beach iliyoko Musoma Mjini pembeni mwa Ziwa Victoria Mkoa wa Mara....

Friday, February 22, 2013

AJIRA KWA MTOTO BADO KITENDAWILI KISICHOPATIWA JIBU?

Saa 4:00 asubuhi muda wa shule mtoto anachunga ng'ombe na mbuzi katika kijiji cha Mugundu wilaya Iramba mkoa wa Singida, nani atalimaliza hi...

MIUNDOMBINU,USAFIRI BADO NI KITENDAWILI KWA WAJAWAZITO MARA?

Ni saa 8:30 mchana Nyangeta Makori ambaye ni mjamzito anatoka kijiji cha Nyambono wilaya ya Musoma vijijini,usafiri unaofaa kwa mjamzito haupo hali iliyomlazimu kuchukua pikipiki na kupita katika barabara mbovu kwa saa nne, huku akisikilizia uchungu kutoka Msoma vijijini mpaka Kituo cha afya cha Manyamanyama wilaya ya Bunda mkoa wa Mara. Alifika saa 11:30 jioni alipokelewa katika kituo cha afya cha Manyamanyama, bila ya kufahamu kama anamapacha...

Thursday, February 21, 2013

LUSIANA MJAMZITO ANAYEPOTEZA DAMU KILA MWEZI

Lusiana Danda (26) alipokuwa na mimba ya miezi nane (Oktoba 2012), alikuwa anatokwa na damu ya mwezi. Hali hii ambayo ni hatarishi kwa mjamzito na mimba yake ilianza wakati ana mimba ya miezi minne, baada ya yeye kuugua malaria.Lusiana, ambaye ni mkulima na mkazi wa kijiji cha Ifinga, Songea, alipata matibabu katika zahanati ya Ifinga. Alivyokutwa na malaria, alipewa dozi ya dawa ya mseto ambayo hakumaliza.“Niliamua kuacha kumeza dawa...