Ukimsikiliza Zaituni Ally (35) anayeishi na virusi vya ukimwi (VVU) kwa miaka saba sasa, machozi yanaweza kukutiririka mashavuni.“Nakula mlo mmoja kwa siku siku nyingine nalala na njaa,”alisema Zaituni.
Siyo hivyo tu. Zaituni ana watoto watatu wenye umri wa miaka 9, 5 na miezi mitatu. Alimzaa mtoto wake wa kwanza, ambaye hivi sasa yuko Mtwara kwa dada yake, akiwa hana maambukizi lakini alijifungua mtoto wa pili na watatu akiwa ameshagunduliwa...